Pamoja na matusi yote ambayo
alishambuliwa na kudhalilishwa Msanii Prezzo na mpenzi wake Starlisha Tillya
al-maarufu CHAGGA BARBIE still ule msemo wa wagombanao ndio wapatanao
ulishika nafasi yake baada ya mwanadada wa Kitanzania
ambaye anaishi Marekani
ameshindwa kumsahau mfalme mswati Prezzo nakuamua kupost picha ambayo aliandika
na maneno kadhaa ambayo yalidhihilisha kuwa wamerudiana kama
inavyoonekana hapo chini katika picha;
STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura
Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha
kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Snura Mushi.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana
ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke
jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi
wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu
wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki
wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli
wowote.
Kazi ipo! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ambaye huwa haishiwi
habari, ameibuka na jipya akidai kuwa akifa leo au kesho basi aagwe
Uwanja wa Taifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda limemtegea sikio.
Wema Isaac Sepetu.
Miss Tanzania huyo wa 2006/07 ambaye anakimbiza kwenye sinema za
Kibongo alifunguka hayo wikiendi iliyopita wakati akiwa safarini
kuelekea jijini Arusha ambapo msanii anayemilikiwa na kampuni ya Wema ya
Endless Fame Production aliyetajwa kwa jina moja la Mirrow alikwenda
kuangusha shoo pande hizo.
Wema aliyasema hayo alipokuwa akichangia mada ya utabiri wa mtoto wa
aliyekuwa mtabiri bingwa, marehemu Sheikh Yahya Hussein, Maalim Hassan
Hussein aliyetabiri kwamba wasanii wengi wenye majina makubwa watakufa
mwaka 2014.
Mwanadada huyo alisema mastaa wengi wameaga dunia na kuagwa kwenye
Viwanja vya Leaders, Kinondoni lakini yeye itakuwa Uwanja wa Taifa.
Alitolea mifano ya waliokuwa mastaa kama Steven Kanumba, Albert
Mangweha ‘Ngwea’, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ na wengine kuwa waliagwa
Leaders lakini kwa namna ambavyo jina lake ni kubwa ndani na nje ya
Bongo viwanja hivyo havitatosha.

“Mimi
nakwambia kabisa, pale Leaders hapatatosha. Kama nikifa leo au kesho,
niagwe Uwanja wa Taifa ili kila mtu apate nafasi. Naamini watu watakuwa
wengi sana so Leaders hapatatosha,” alisema staa huyo mkubwa anayeminya
kilamalavidavi na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Ijumaa Wikienda lilipododosa kwa marafiki zake wa karibu lilitonywa
kwamba tayari jambo hilo alishawaeleza na kwamba aliomba iwe hivyo.
Mbali na wasanii, Maalim Hassan alitabiri pia kuwa mwaka huu kuna
mwanasiasa mkubwa atakufa na utakuwa msiba wa kitaifa, vifo vya
wanahabari na malumbano makubwa juu ya serikali tatu.
Wiki iliyopita ilijaa simanzi baada ya kufariki dunia kwa watu
maarufu kama mchekeshaji wa Futuhi ya Star TV, Omary Majuto ‘Mzee Dude’,
mpiga ngoma wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Soud Mohamed
‘MCD’, mwigizaji wa Bongo Movies, Victor Peter na mtangazaji wa East
Africa Radio, Kenneth Kidago Lyanga.
She started yesterday and she is showing no sign of own dow.Her goal is to get her bikini body back...
Sexy belly..Like JLO...
Akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za
udiwani kata ya malindo wilayani rungwe,Sugu amesema yeye kajenga
ghorofa jijini mbeya na wala si mpangaji kama adhanivyo nape pia
kamwambia kinana kuwa karibu na wakulima ni kuwapa mbolea na si kupiga
picha na wakulima kisha kutoa gazetini. Akizungumzia hoja ya nape
aliyesema sugu ni mpangaji jimbo la mbeya mjini sugu amekosoa hoja
hiyo,pia kuhusu mgogoro ndani ya chadema kasema imebaki historia ila
wana ccm wana gogoro linalokua kila siku.hakika nguvu ya umma hakuna kulala!